fabian delph ni chaguo sahihi man city?
City haitegemei kuwa na Lampard, ukimwangalia yaya toure umri unazidi kwenda, fernado ni mzito si rahis kumudu aina ya mpira ya viungo wepesi zaidi hususani wanaopatikana Arsenal, Man United na Liverpool. lakini delph ana miaka 25 pekee ukilinganisha na kiwango chake ni hazina ya msingi katika kikosi cha man city.
kama manueli pellegrini ameweka mpango wa kumsajili kiungo huyo namwunga mkono, nakumbuka nusu fainali ya FA cup dhidi ya liverpool kiungo huyu alivyofanya vizuri hakika ni aina ya kiungo ambaye unahitaji kuwa naye kwenye timu. anastahili kucheza city, kama city haitafanikiwa kuwa na wilshere fabian delph ni mbadadala tosha.
kama atacheza na fernandinho na yaya toure akawa huru zaidi na david silva uwanjani nadhani city itarudia kwenye makali yake, hii itamfanya yaya toure afikirie mbinu zaidi za kuipa timu ushindi kama alivyofanya msimu wa 2013/14 hii italeta changamoto kubwa ya kuwania taji la barclays kwa wale vigogo wanne wa juu.
bila shaka huyu atakuwa nyota bora kati ya miamba bora pale Etihad nina iman city ikiwa na delph itakuwa na safu bora kiungo itakayoleta changamoto kubwa kwa wapinzani, na hii inaweza kuifanya city kuwa na kikosi bora msimu 2015/16 na kujitengenezea nafasi ya kuwa bingwa.
No comments:
Post a Comment