Saturday, June 27, 2015

Ni kitu gani wanahitaji liverpool wawe bora 2015/16

Liverpool imekalisha usajili wa kiungo mshambualiji kutoka hoffehm ya ujermani ambaye ameungana na James Milner kati ya wachezaji wapya waliosjailiwa katika timu hiyo, Firmino 23, anaweza kucheza namba zote zote za mbele akiwa kama fowadi, wing-midfilder na kiungo mshambuliaji.

Liverpool sasa itakuwa na James milner, Daniel Sturridge, Divock Origi, Phillipe Coutinho, Roberto Firmino na Raheem Sterling kama hatoondoka klabuni hao wote wanategemewa kuongoza safu ya ushambuliaji katika kikosi cha brendan rodgers. kutokana mahitaji ya breandan rodgers ina wezekana akafanikiwa katika msimu ujao wa ligi kutoka na wachezaji hao wote kuwa na kasi katika kushambulia kama anavyohitaji.

Lakini liverpool haitakuwa na steven gerrard msimu mpya hivyo inabidi wapate kiungo mkabaji mwingine ambaye ataweza kudumisha ulinzi wa timu hiyo, hicho ni kibarua kigumu kwa Rodgers ingawa amekuwa na mipango ya kumsajili kiungo makabajji wa tiu ya real madrid Asier Illaramendi.

Licha ya safu ya kukaba lakini rodgers bado anahitaji mbadala wa Suarez, msimu wa 2014/15 umeonyesha ni namna gani Sturridge anahitaji mtu wa kumwongoza katika safu ya kushambulia kama ilivyokuwa yeye na Suarez, na ndiyo maana Rogers anaisaka kwa udi na uvumba sahihi ya mshambuliaji wa sevilla Carlos Bacca huku akiendelea kuifuatilia sahihi ya mshambuliaji wa Aston villa Christian Benteke kwa ajili ya kuimalisha safu a ushambuliaji katika timu hiyo ambayo haikufanya vizuri kama alivyokuwa Suarez.

Kama Liverpool itakuwa na kiungo imara kama enzi ya Mascherano na kupata mshambuliaji mkali kama Carlos Bacca nadhani tatizo la Liverpool litakuwa limeisha rasmi nahitaji maoni yako msomaji kwa upande wangu nadhani Liverpool inatkiwa kuziba mapengo hayo ili iweze kurudi kwenye ubora wake.


No comments:

Post a Comment