Sunday, June 21, 2015

sielewi kabisa ule mpira pale taifa stars
Na Kapinga EMANUELI
 jana nimeshangazwa na namna kocha wa timu ya taifa maarufu kama taifa stars alivyowapanga viungo ndani ya kikosi chetu, kwanza ni frank domayo, Erasto Nyoni na Amri kiemba alafu baadae tukawa na jonas mkude, Erasto Nyoni na Rashid Mandawa tukiwa tumeshafungwa goli mbili.
ndiyo mana nimeanza na kusema kuwa sielewi maana kama umeshafungwa goli mbili kuna haja gani ya kuwa na viungo wawili wagumu ndani ya timu, labda tungekuwa tunajitoa kama wenzetu Uganda tungepata goli la kuongoza tungetumia aina hiyo ya mfumo kujitoa wapinzani wasipate mwanya wa kusawazisha.
kocha Jose Mourinho ndiye fundi wa kupaki basi na kutumia zaidi viungo wakaidi ndani ya timu lakini wachezaji wake wanajituma, utakuta ana matic au na ramires lakini angalia kuanzia fabrigas, hazard, oscar au willian na diego costa au remy ni tofauti nna sisi. kama Mourinho angeona aina ya mpira tuliocheza hakika angesema sisi ni vichaa au wendaazim.
hata mourinho huweka wakina xhuma na kupunguza washambuliaji kwa sababu huwa ameshapata anachokiitaji mfano mzuri ni ushindi dhidi ya manchester united pale stamford bridge. mimi binafsi sikuona sababu ya kuwa na viungo wagumu kiasi hicho kwa sababu kwanza hatuwezi kumiliki mchezo licha ya kuwa na viungo wengi wengi kiasi hicho lakini pili tumeruhusu magoli matatu hakuna maana ya kuwa na mfumo huo.
kuna haja ya kuwa na kiemba ambaye hana uhakika wa kucheza katika kwenye klabu yake, free role ambaye hana msaada hawezi kumiliki mipira, na kuiunga timu dhidi ya washabuliaji wake, sioni kama kuna sababu lazma Erasto Nyoni acheze kwenye sehemu ya kiungo ikiwa  ikiwa timu inaweza kuwa na mkude au aina ya mtu kama shabani nditi.

No comments:

Post a Comment