Na
EMANUELI KAPINGA.
Mara nyingi tunachagua viongozi ambao hawawezi
kuwajibika katika soka, mfano mzuri ni kutoka Simba sports kamati ya usjili ina
mzaa na maendeleo ya klabu,Simba iliingia kwenye mgogoro na Ramadhani Singano maarufu
kama “messi” hii ni wazi kuwa hatuna watu makini wakushughulika na mikataba ya
wachezaji. Katika nchi zilizoendelea huboresha mikataba ya wachezaji mwaka au
miezi sita kabla ya kuelekea ukingoni kama wanahisi mchezaji ana thamani kwao
hii ni kwa ajili ya kupata faida zaida kwa timu zikatakomwitaji kwa kuwa
mkataba uko wazi.
Simba wasisikitike wamwache Singano aondoke, hakuna
namna kwamba alikuwa na thamani kwao au walihiitaji kufanya kupata faida
kupitia yeye hivyo hakuwa na thaman kwao wamwache aende au waweke pesa mezani
waache ubabaishaji.
Nimesikitika kusikia eti Azam Tv ndiyo chanzo cha
kushuka kwa mapato kutokana na watu kutofika uwanjani, tuache visingizio
ambavyo havina msingi na badala yake tuangalie tatizo liko wapi, kuna vituo
maarufu dunian kama Sky Sports, Super Sport
zinarusha ligi bora ulaya na mapato katika klabu hizo ni mengi.
Adui wa yote ni sisi wenyewe tuangalie tatizo letu
liko wapi. Aina ya mpira unaochezwa hauvutii watazamaji kwenda viwanjani na
hivyo wachezaji hupendelea kujaa viwanjani dhidi ya mechi tatu kati ya Simba,
Azam na Yanga. Katika vituo vya azam watazamaji wengi pia hushindwa kumaliza
baadhi ya mechi nyingi kutokana na soka kukosa mvuto.
Juzi katika tuzo za soka Tanzania kumezua vituko, mimi
binafsi siwelewi Shabani Kado amewezaje kuwa goli kipa bora uku akiwa ametemwa
na timu yake ya Coastal Union, ni wapi duniani kipa bora amewahi kutemwa kwenye
timu yake, na yeye Mbwana Makata amewezaje kuwa kocha bora mbele Pluijim na
Juma Mwambusi wa mbeya city tujiulize adui yetu ni nani ili tuweze kuleta
mabadiliko katika soka letu la Tanzania.
Binafsi naumia kuyaona haya hatukuzi bali tunaua soka,
hebu tuache ujanja ujanja, tuwe wa wataalam tuhamasishe soka bora, tusijali
pesa kuwaweka viongozi ambao hawaelewi maana ya usajili au kanuni za soka au
vyanzo vya maendeleo katika timu eti kisa ni shabiki wa muda mrefu na analipia
kadi ya uanachama.
No comments:
Post a Comment